text
stringlengths
3
16.2k
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI NAIROBI, KENYA RAIA wa Rwanda Desire Muhinyuza atasherehekea Mwaka Mpya 2024 akiwa na amani na utulivu moyoni, baada ya Serikali ya Kenya kuamuru arudishiwe Dola 2.6 milioni (sawa na Sh400 milioni) zilizokuwa zimetwaliwa na Polisi kufuatia mzozo wa umiliki wa kampuni ya biashara ya kimtandao kati yake na mfanyabiashara wa humu nchini Bw Kirimi Koome. Hatua hii ya serikali ni muhimu katika kuimarisha imani ya wawekezaji wanaotoroka nchini mara baada ya kulaghaiwa na baadhi ya Wakenya. Akiamuru Bw Muhinyuza akabidhiwe kitita hicho, hakimu mwandamizi katika mahakama ya Milimani, Nairobi Bi Dolphina Alego alisema Mahakama Kuu mnamo Desemba 27, 2023, ilimtambua mwekezaji huyo kuwa ndiye mwenye kampuni ya Stay Online Limited (SOL) aliyokuwa amenyang’anywa na Bw Koome kwa njia ya ujanja na ufisadi. Bi Alego alisema Jaji Alfred Mabeya, ambaye ni mkuu wa kitengo cha biashara katika Mahakama Kuu, alimtambua Bw Muhinyuza kuwa ndiye mmiliki wa SOL, aliyokuwa amelaghaiwa na Bw Koome mnamo Aprili 14, 2023. Jaji Mabeya alisema katika uamuzi huo wa kihistoria kwamba Bw Koome alitumia ukora na ulaghai kujisingizia na kujitambua kuwa mmiliki wa SOL ilhali alikuwa ameteuliwa na Bw Muhinyuza aiandikishe kwa niaba yake. “Bw Koome aliteuliwa na Bw Muhinyuza aandikishe SOL, Kenya kwa niaba yake, lakini akajisingizia kuwa yake na kupotosha idara ya usajili wa kampuni katika afisi ya Mwanasheria Mkuu,” Bi Alego alisema. Punde tu baada ya kuandikisha SOL, Kenya wafanyabiashara kutoka Canada, Estonia, Zambia, Tanzania, Uganda, na Kenya waliwekeza zaidi ya Dola 2.6 milioni (Sh400 milioni) katika biashara hiyo ya jukwa la mtandaoni. Kuona kwamba amepokonywa kampuni ya SOL, Bw Muhinyuza alilalamika kwa polisi kwamba ametapeliwa kampuni na pesa na Bw Koome ndipo, idara ya uchunguzi wa jinai (DCI) ikafika kortini na kupata agizo la kutwaa pesa hizo sizipotee. Na wakati huo huo Bw Muhinyuza akalalamikia idara ya usajili wa kampuni katika afisi ya mwanasheria mkuu kwamba Bw Koome alificha ukweli kuhusu umiliki wa SOL. Pia Bw Muhinyuza kupitia mawakili Danstan Omari, Shadrack Wambui, Sophie Nekesa, Ronald Momanyi na Aranga Omaiyo alimshtaki Bw Koome katika mahakama kuu akiomba ashurutishwe arudishe kampuni na pesa za wateja walioekeza katika SOL, Kenya. Baada ya kutathmini ushahidi uliowasilishwa na Bw Omari, Jaji Mabeya alifikia uamuzi kwamba SOL ni yake Bw Muhinyuza. Alisema mwekezaji huyo aliekeza USD ($)129,000 katika SOL na Bw Koome “hakutoa hata senti moja kufanikisha biashara na usajili wake.” Jaji huyo alimwagiza Bw Koome anayeshtakiwa mbele hakimu mkazi Bw Ben Mark Ekhubi kwa kula njama za kumlaghai Bw Muhinyuza kiasi cha Dola 2.6 milioni na wizi wa Dola 100,000 arudishe pesa hizo. Ijumaa ,viongozi wa mashtaka Bi Dorcus Rugut na James Gachoka walisema ijapokuwa Bw Koome anadai pesa hizo ni zake “hana mamlaka yoyote juu ya pesa hizo.” Bi Rugut alisema Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Igonga ameamuru polisi wamrudishie Bw Muhinyuza kiasi hicho Dola 2.6 milioni. Bi Alego alisema serikali imeagiza pesa hizo zirudishwe kwa mwekezaji huyo aendelee na biashara na kubuni ajira kwa wakenya. Kabla ya polisi kuagizwa kurudisha pesa hizo Bw Koome alipinga ombi hilo akisema “apewe muda wa wiki mbili atafute wakili awasilishe ombi la kuzuia kutwaliwa kwa pesa hizo na Muhinyuza.” Bw Koome alisema : “nimewatimua kazini mawakili Cliff Ombeta, Jackson Omwanza na hivyo nahitaji muda wa kumtafuta wakili mwingine kwa vile sielewi ombi hili la DPP na madhara yake katika kesi hii inayonikabili.” Mahakama iliombwa na wakili Danstan Omari isitilie maanani ombi la Bw Koome kwa vile “pesa anazodai sio zake.” Bi Rugut alisema DPP hapingi pesa hizo zilizokuwa zimezuiliwa kama ushahidi katika kesi inayomkabili Bw Koome. Bi Rugut alisema Desemba 27, 2023, Bw Koome hajakata rufaa kupinga uamuzi wa kumng’oa katika kampuni ya SOL na agizo la kulipa fidia na kurudishia Muhinyuza Dola 100,000 alizomdanganya zilikuwa za kulipia kodi biashara ya SOL lakini “akazitia kibindoni.” Bi Alego alielezwa kesi inayomkabili Bw Koome ni kwamba alikula njama za kumlaghai Bw Muhinyuza kiasi Dola 2.6 milioni na wizi wa Dola 100,000. Mahakama ilikubalia ombi la DPP na kuagiza pesa hizo arudishiwe Muhinyuza. Sasa Bw Koome atapambana na hali yake na kesi ya ufisadi inayomkabili. Kesi inayomkabili Bw Koome itaanza kusikilizwa Februari 9, 2023. Alikana mashtaka manne ya ufisadi na wizi na yuko nje kwa dhamana ya pesa taslimu Sh500,000 You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
It looks like nothing was found at this location. Maybe try one of the links below or a search? Try looking in the monthly archives. 🙂 © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
It looks like nothing was found at this location. Maybe try one of the links below or a search? Try looking in the monthly archives. 🙂 © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na CHARLES WASONGA MAGAVANA nchini sasa wanaweza kupumua baada ya maseneta kulegeza msimamo wao na kukubali mgao wa Sh316.5 bilioni kwa kaunti jinsi ilivyopendekezwa na wabunge na serikali kuu. Hatua hiyo ya busara iliyochukuliwa Alhamisi sasa imemaliza mvutano kuhusu suala hilo na kaunti zinatarajia kuanza kupokea fedha hizo kuanzia wiki ijayo bunge la kitaifa litakaporejelea vikao vyake. Mswada mpya wa ugavi wa fedha (DoRB) uliopendekeza kiasi hicho cha fedha sasa utawasilishwa katika seneti ili upitishwe kabla ya kutiwa saini na Rais Uhuru Kenyatta.?Awali, maseneta walikuwa wamependekeza kaunti zipewe mgao wa Sh335.7 bilioni katika bajeti ya sasa ya mwaka wa kifedha wa 2019/2020. Kiasi hicho ndicho kilikuwa kimewekwa na Tume ya Ugavi wa Rasilimali (CRA). Lakini maseneta jana walilegeza msimamo baada ya mkutano wao uliotishwa na Spika wao Ken Lusaka.?Kwenye kikao na wanahabari katika majengo ya bunge, kiongozi wa wengi Kipchumba Murkomen alisema wamefanya “uamuzi huo mchungu” ili kuzuia uwezekano wa kusitishwa kwa shughuli muhimu katika kaunti. “Fedha hizo hazitoshi, lakini ni afadhali na seneti itaendelea kupigania fedha zaidi wakati mwingine. Seneti haitaruhusu ugatuzi ambao ndio nguzo kuu ya Katiba yetu kuhujumiwa kupitia njama fulani,” Bw Murkomen akasema. Mvutano umekuwa ukiendelea kuhusu suala hilo tangu Juni, hali iliyopelekea bajeti ya mwaka huu kusomwa kabla ya kupitishwa kwa mswada wa ugavi wa fedha.?Awali, bunge la kitaifa lilipendekeza mgao wa Sh310 bilioni kwa kaunti, lakini baadaye likaongeza kiasi hicho hadi 316.5 bilioni baada ya kamati ya maridhiano kuundwa kutafuta muafaka kuhusu suala hilo. Nao maseneta walipunguza kiasi cha fedha walichopendekeza hadi Sh327.7 bilion, ndipo wakakosa kuelewana na wabunge. Kutoelewana huko ndiko kulisababisha Waziri wa Fedha aliyesimamishwa kazi Henry Rotich kusoma bajeti, Juni 13, iliyotenga Sh310 bilioni kwa kaunti.? Na mwezi jana, Bunge la Kitaifa, kupitia kamati kuhusu bajeti, lilitayarisha mswada mwingine wa ugavi wa fedha likizitengea serikali Sh316.5 bilioni, kiasi ambacho Rais Kenyatta aliunga mkono. Kiongozi wa taifa alisema serikali haina fedha za kuongeza serikali za kaunti. Akasema alipohudhuria mazishi ya mamake mwanasiasa Peter Kenneth: “Nyinyi wabunge mwaweza kupunguza mishahara yenu na mzipe kaunti pesa zaidi. Lakini mimi sina pesa za kuwaongezea!”?Mvutano kuhusu suala hilo ulichochea magavana kwenda katika Mahakama ya Juu wakitaka ushauri kuhusu suala hilo. Hata hivyo, majaji wa mahakama hiyo, wakiongozwa na Jaji Mkuu David Maraga, walisema suala hili linaweza tu kutatuliwa na mabunge yote mawili sio mahakamani. ?Bw Maraga aliwashauri maspika Justin Muturi na Lusaka kuunda kamati nyingine ya maridhiano kutanzua mvutano huo. Hata hivyo, kikao cha kwanza cha kamati hiyo, kilichofanyika katika ukumbi wa County, Nairobi, wiki jana kiligeuka uwanja wa vita vya maneno kati ya maseneta na wabunge. Wawikilishi wa mabunge hayo mawili walishikilia misimamo yao ya awali na hivyo kukosa kuelewana.?Hii ndio maana wiki jana mwenyekiti wa Baraza la Magavana (CoG) Wycliffe Oparanya alitangaza kuwa serikali zote za kaunti zitasitisha shughuli ifikapo tarehe 16 mwezi huo ikiwa muafaka hautapatikana kuhusu suala hilo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na WAANDISHI WETU SERIKALI imewazima wanasiasa wanaotetea wakazi walioagizwa kuhama msitu wa Mau, Kaunti ya Narok, ikisema hatua hiyo ilipitishwa na Baraza la Mawaziri na itatekelezwa kikamilifu ilivyopangwa. Msemaji wa serikali, Kanali mstaafu Cyrus Oguna, Alhamisi alieleza kwamba serikali hailengi msitu wa Mau pekee bali wakazi wanaoishi katika misitu ya Mlima Kenya na Aberdare pia watahamishwa. Kauli hii ililenga viongozi kutoka Rift Valley ambao wamekuwa wakiikosoa hatua ya serikali ya kuwafurusha wakazi kutoka msitu wa Mau wakimlaumu Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko kwa kutumia mamlaka yake vibaya. Seneta wa Elgeyo Marakwet, Bw Kipchumba Murkomen, alidai kwamba serikali haikuwa imetoa agizo la kufurusha wakazi kutoka Mau akisema Bw Tobiko alikuwa akitumiwa na watu wanaotaka kumzuia Naibu Rais kushinda urais kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2022. Bw Murkomen aliongoza wanasiasa wengine kumtaka Rais Uhuru Kenyatta kujitokeza na kueleza iwapo amempa Bw Tobiko agizo la kufurusha wakazi kutoka msitu huo. Jana, Bw Oguna alisema wakazi hao watahamishwa sawa na wanaoishi katika misitu mingine nchini na hakuna njama fiche jinsi wanasiasa hao walivyodai. Hata hivyo, alisema shughuli hiyo itafanywa kwa njia ya utu. “Ufurushaji wa watu kutoka msitu wa Mau lazima utekelezwe ili kuokoa nchi yetu lakini hilo litafanywa kwa njia ya utu. Neno muafaka kutumia hapa ni kuhamisha familia hizo na sio kuzitimua,” alisema Bw Oguna akihutubia wanahabari katika kikao cha kila Alhamisi. Alisisitiza kuwa serikali inaelewa changamoto zilizopo na italinda hadhi ya watu. Serikali inalenga kuwaondoa wakazi wanaozidi 60,000 kutoka msitu wa Mau. Iliwapa makataa ya siku 60 kuondoka, makataa yatakayokamilika Oktoba 30 mwaka huu. Tayari watu wameanza kuondoka katika msitu huo licha ya wanasiasa kuwataka kukaidi agizo la serikali. Maeneo ambayo watu wamehama ni Sierra Leone, Enokishomi, Enoosokon, Nkaroni, Nkoben, Ilmotiok, Ololung’a na Sisian. Wakazi hao walisema waliamua kuhama wakiogopa maafisa wa usalama ambao wametumwa eneo hilo. Ripoti za Benson Matheka, Anita Chepkoech na George Sayagie You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na BENSON MATHEKA Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, amepata nguvu na ushawishi mkubwa serikalini, licha ya kukanusha kwamba ameacha majukumu yake kama kiongozi wa upinzani. Kwa kila hali, Bw Odinga anaonekana kuwa na usemi serikalini huku akishauriana na maafisa wakuu, wakiwemo mawaziri, wakuu wa idara mbali mbali, mabalozi na kukagua miradi ya maendeleo. Afisi yake ya Capitol Hill jijini Nairobi, imekuwa kama madhabahu huku akitembelewa na maafisa wa serikali kuu na za kaunti. Isitoshe, amewahi kupokea na kushauriana na kiongozi wa nchi ya kigeni katika afisi hiyo. Jana, alishauriana na viongozi kutoka kaunti za Kisii na Nyamira walioongozwa na magavana James Ongwae na John Nyangarama. pamoja na seneta wa Kisii Prof Sam Ongeri. “Viongozi kutoka eneo la Kisii leo walimtembelea kiongozi wa chama @RailaOdinga katika afisi yake Capital Hill ambapo walijadili masuala yenye umuhimu wa kitaifa,” chama cha ODM kilisema kwenye ujumbe wa Twitter. Wadadisi wanasema kuna kila dalili kwamba Bw Odinga alipata nguvu mpya kufuatia muafaka kati yake ya Rais Uhuru Kenyatta waliotangaza Machi 9 2019. “Yeye na familia yake waliongezewa walinzi na imekuwa vigumu kwa baadhi ya washirika wake kumtembelea walivyokuwa wamezoea kabla ya muafaka huo,” asema mbunge mmoja wa ODM ambaye hakutaka tutaje jina kwa sababu ya uhusiano wake na kiongozi huyo. Baadhi ya mawaziri ambao wamemtembelea katika afisi yake au kukutana naye kushauriana ni Peter Munya wa Viwanda, Profesa Margaret Kobia wa Utumishi wa Umma, Mwangi Kiunjuri wa kilimo na James Macharia wa uchukuzi. Aidha, amekuwa akishirikiana na waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i, waziri wa michezo Amina Mohammed na waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa. Katika kile kinachoashiria kwamba anashawishi maamuzi ya serikali, Bw Odinga amekuwa akitoa matamshi ya kuunga sera za serikali na kila anakoenda, anapokewa kwa heshima zote za afisa wa serikali. Wadadisi wanasema sio siri kwamba Bw Odinga anafahamu, kushawishi au kuhusika na maamuzi ya serikali tangu muafaka wake na Rais Kenyatta. “Amekuwa akiweka wazi kuwa yeye na Rais Kenyatta waliamua kushirikiana kufanikisha ajenda na sera za serikali. Amenukuliwa mara kadhaa akisema yeye na Rais Kenyatta wameamua kupigana na ufisadi. Mtu hawezi kufanikisha ajenda za serikali akiwa nje ya serikali,” asema mdadisi wa siasa, Duncan Wafula. Kulingana na Bw Munya, mawaziri wanashauriana na Bw Odinga kwa sababu ya ushirikiano wake na Rais Kenyatta wa kuunganisha Wakenya. “Wakati Rais Kenyatta na Bw Odinga walizindua kamati ya uwiano (BBI), ilikuwa ishara kwamba tunapaswa (mawaziri) kushirikiana na Bw Odinga kwa sababu hata yeye ni Mkenya,” Bw Munya aliambia Taifa Leo baada ya kuzuru Urusi akiwa na Bw Odinga. Mawaziri wote waliagizwa kushirikisha BBI katika ajenda za serikali ishara kuwa wanapaswa kumtambua na kushirikiana na Bw Odinga. Kulingana na msemaji wa Bw Odinga, Dennis Onyango, kiongozi huyo wa ODM, hana wadhifa wowote serikalini lakini maafisa wakuu huwa wanatafuta ushauri kutoka kwake hasa kuhusu masuala anayoelewa vyema kama miundomisingi. Mnamoi Julai, Bw Odinga alizuru maeneo yanayojengwa vituo maalumu vya kiuchumi jijini Kisumu akiwa na Waziri Macharia. Wiki jana, alizuru mradi wa kilimo wa Galana Kulalu akiandamana na maafisa wa serikali. Ametumia mamlaka yake kuhakikisha ngome yake ya Nyanza na hasa jiji la Kisumu imepata maendeleo tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza cha utawala wa Jubilee. Aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale alishangazwa na jinsi Bw Odinga anashawishi serikali kuzindua miradi ya maendeleo Nyanza. Aidha, wanachama wa ODM wameteuliwa katika bodi za mashirika ya serikali akiwemo afisa mkuu mtendaji wa uliokuwa muungano wa NASA Norman Magaya (bodi ya kudhibiti filamu) na mwanaharakati wa ODM David Osiany (Bodi ya kampuni ya sukari ya Chemelil). Katika ziara zake nje ya nchi, Bw Odinga amekuwa akipokewa na mabalozi wa Kenya na kupewa heshima zote za kiongozi wa serikali tofauti na awali alipozuiwa kutumia eneo la watu mashuhuri katika viwanja vya ndege nchini. Hali ni sawa anapozuru maeneo tofauti ambapo amekuwa akipokewa na makamishna wa kaunti na usalama kuimarishwa. Magavana wengine ambao walimtembelea ni Ann Waiguru wa Kirinyaga, Granton Samboja wa Taita Taveta na Alfred Mutua wa Machakos. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na MASHIRIKA MAUAJI yanayolenga raia wa kigeni nchini Afrika Kusini yamezua ghadhabu katika mataifa mbalimbali ya Afrika huku idadi ya waliouawa kinyama ikifikia watu saba. Umoja wa Afrika (AU) ulishutumu vurugu dhidi ya raia wa kigeni zinazoendelea jijini Johannesburg, huku ukisema kuwa wafanyabiashara ambao wamepata hasara katika machafuko hayo wanafaa kulipwa fidia. Watu wasiopungua 80 wamekamatwa kufuatia vurugu hizo ambapo mamia ya vijana walivamia na kupora biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni. Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa AU Moussa Faki Mahamat, alipongeza serikali ya Afrika Kusini kwa kuwakamata wahusika wa vurugu hizo. “Serikali ya Afrika Kusini haina budi kulinda maisha na mali ya Waafrika wenzao. Umoja wa Afrika uko tayari kusaidia,” akasema Bw Faki. Rais wa Zambia Edgar Lungu aliitaka serikali ya Afrika Kusini kukomesha vurugu hizo mara moja. “Nawasihi raia wa Zambia humu nchini na ughaibuni kutowadhuru raia wa Afrika Kusini walio karibu nao. Tulaani unyama unaotendeka nchini humo bila kuzua fujo,” akasema Rais Lungu kupitia mtandao wa Facebook. Rais Lungu alitoa kauli hiyo baada ya raia wa Zambia kuandamana jijini Lusaka na kupora maduka yanayomilikiwa na raia wa Afrika Kusini. Shirikisho la Kandanda nchini Zambia (Faz) lilifutilia mbali mechi ya kirafiki baina ya timu ya nchi hiyo (Chipolopolo na ile ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) iliyofaa kuchezwa Jumamosi jijini Lusaka. Shirikisho hilo lilifutilia mbali mechi hiyo baada ya raia kulishinikiza kuitupilia mbali kama njia mojawapo ya kupinga mauaji ya kinyama na uharibifu wa mali jijini Johannesburg. Wakati huo huo, polisi nchini Nigeria jana walidumisha usalama katika biashara zinazomilikiwa na raia wa Afrika Kusini jijini Abuja kutokana na hofu kwamba huenda zikavamiwa. Polisi walishika doria nje ya maduka na afisi za mtandao wa simu wa MTN unaomilikiwa na Afrika Kusini. Mtandao wa MTN, hata hivyo, ulikuwa umefunga afisi zake zote jijini Abuja kwa kuhofia kushambuliwa. “Tumefunga kwa kuhofia usalama wa wafanyakazi na wateja wetu,” ikasema notisi iliyobandikwa nje ya afisi hizo. Jumanne, watu waliokuwa na ghadhabu walivamia na kupora mali katika duka linalomilikiwa na raia wa Afrika Kusini jijini Lagos, Nigeria. Wasanii kadhaa, akiwemo mwanamuziki Tiwa Savage wa Nigeria wamefutilia mbali matamasha waliyofaa kutumbuiza nchini Afrika Kusini. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumanne alilaani vurugu hizo huku akisema kuwa zinatia doa sifa ya Afrika Kusini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na JOSEPH WANGUI WABUNGE wa mrengo wa ‘Kieleweke’ kutoka Mlima Kenya wanaitaka Ikulu kueleza ikiwa Rais Uhuru Kenyatta huwa anampa Naibu Rais William Ruto pesa za kutoa kwenye michango ya makanisa anayohudhuria. Wikendi iliyopita, Dkt Ruto alitoa jumla ya Sh7.5 milioni kwenye harambee za makanisa manne katika kaunti za Nyeri na Kirinyaga, akisema Sh2 milioni zilikuwa mchango kutoka kwa Rais Kenyatta. Mjini Nyeri, alitoa Sh3 milioni kwa kanisa la ACK St Paul’s Kariki, Othaya, Sh2 milioni zikiwa mchango wake binafsi huku Sh1 milioni zikiwa mchango wa Rais Kenyatta. Vile vile, alitoa Sh1 milioni kwa kanisa la AIPCA Narumoru katika eneo la Kieni. Katika Kaunti ya Kirinyaga, alitoa Sh3 milioni kwa Kanisa la Katoliki la Parokia ya Kangaita, mjini Kerugoya. Kwenye mchango huo, Sh2 milioni zilikuwa mchango wake binafsi, huku Sh1 milioni zikiwa mchango kutoka kwa Rais Kenyatta. Baada ya hapo, alielekea katika Kanisa la Full Gospel Gichugu, alikotoa Sh500,000. Wakiongozwa na Mbunge Maalum Maina Kamanda, wanasiasa hao walisema Rais Kenyatta anapaswa kueleza ikiwa ndiye huwa anatoa michango hiyo kama vile Dkt Ruto amekuwa akidai. “Uhuru anapaswa kutwambia ikiwa yeye ndiye amekuwa akimtuma Dkt Ruto na michango ya Sh1 milioni katika kila hafla ya kuchangisha pesa anayohudhuria. Sababu kuu ni kwamba amegeuza makanisa katika eneo la Kati kuwa majukwaa ya kufanyia siasa,” akasema Bw Kamanda, ambaye amekuwa akiongoza kampeni dhidi ya Dkt Ruto. Kulingana na mwanasiasa huyo mkongwe, Dkt Ruto hatapata uungwaji mkono wowote kwa kumpinga Rais Kenyatta, hasa kwenye mipango yake kama Jopo la Maridhano (BBI). Kwenye ziara yake katika Kaunti ya Nyeri, Dkt Ruto alitaja jopo hilo kama upotezaji muda. “Eneo la Kati halitadanganyika kumfuata. Tuko kila mahali tukijenga daraja la maelewano,” akasema Bw Kamanda. Kauli yake iliungwa mkono na wabunge Ngunjiri Wambugu (Nyeri Mjini) na Maoka Maore (Igembe Kaskazini). You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA