text
stringlengths 3
16.2k
|
---|
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI |
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MUNGUTI NAIROBI, KENYA RAIA wa Rwanda Desire Muhinyuza atasherehekea Mwaka Mpya 2024 akiwa na amani na utulivu moyoni, baada ya Serikali ya Kenya kuamuru arudishiwe Dola 2.6 milioni (sawa na Sh400 milioni) zilizokuwa zimetwaliwa na Polisi kufuatia mzozo wa umiliki wa kampuni ya biashara ya kimtandao kati yake na mfanyabiashara wa humu nchini Bw Kirimi Koome. Hatua hii ya serikali ni muhimu katika kuimarisha imani ya wawekezaji wanaotoroka nchini mara baada ya kulaghaiwa na baadhi ya Wakenya. Akiamuru Bw Muhinyuza akabidhiwe kitita hicho, hakimu mwandamizi katika mahakama ya Milimani, Nairobi Bi Dolphina Alego alisema Mahakama Kuu mnamo Desemba 27, 2023, ilimtambua mwekezaji huyo kuwa ndiye mwenye kampuni ya Stay Online Limited (SOL) aliyokuwa amenyang’anywa na Bw Koome kwa njia ya ujanja na ufisadi. Bi Alego alisema Jaji Alfred Mabeya, ambaye ni mkuu wa kitengo cha biashara katika Mahakama Kuu, alimtambua Bw Muhinyuza kuwa ndiye mmiliki wa SOL, aliyokuwa amelaghaiwa na Bw Koome mnamo Aprili 14, 2023. Jaji Mabeya alisema katika uamuzi huo wa kihistoria kwamba Bw Koome alitumia ukora na ulaghai kujisingizia na kujitambua kuwa mmiliki wa SOL ilhali alikuwa ameteuliwa na Bw Muhinyuza aiandikishe kwa niaba yake. “Bw Koome aliteuliwa na Bw Muhinyuza aandikishe SOL, Kenya kwa niaba yake, lakini akajisingizia kuwa yake na kupotosha idara ya usajili wa kampuni katika afisi ya Mwanasheria Mkuu,” Bi Alego alisema. Punde tu baada ya kuandikisha SOL, Kenya wafanyabiashara kutoka Canada, Estonia, Zambia, Tanzania, Uganda, na Kenya waliwekeza zaidi ya Dola 2.6 milioni (Sh400 milioni) katika biashara hiyo ya jukwa la mtandaoni. Kuona kwamba amepokonywa kampuni ya SOL, Bw Muhinyuza alilalamika kwa polisi kwamba ametapeliwa kampuni na pesa na Bw Koome ndipo, idara ya uchunguzi wa jinai (DCI) ikafika kortini na kupata agizo la kutwaa pesa hizo sizipotee. Na wakati huo huo Bw Muhinyuza akalalamikia idara ya usajili wa kampuni katika afisi ya mwanasheria mkuu kwamba Bw Koome alificha ukweli kuhusu umiliki wa SOL. Pia Bw Muhinyuza kupitia mawakili Danstan Omari, Shadrack Wambui, Sophie Nekesa, Ronald Momanyi na Aranga Omaiyo alimshtaki Bw Koome katika mahakama kuu akiomba ashurutishwe arudishe kampuni na pesa za wateja walioekeza katika SOL, Kenya. Baada ya kutathmini ushahidi uliowasilishwa na Bw Omari, Jaji Mabeya alifikia uamuzi kwamba SOL ni yake Bw Muhinyuza. Alisema mwekezaji huyo aliekeza USD ($)129,000 katika SOL na Bw Koome “hakutoa hata senti moja kufanikisha biashara na usajili wake.” Jaji huyo alimwagiza Bw Koome anayeshtakiwa mbele hakimu mkazi Bw Ben Mark Ekhubi kwa kula njama za kumlaghai Bw Muhinyuza kiasi cha Dola 2.6 milioni na wizi wa Dola 100,000 arudishe pesa hizo. Ijumaa ,viongozi wa mashtaka Bi Dorcus Rugut na James Gachoka walisema ijapokuwa Bw Koome anadai pesa hizo ni zake “hana mamlaka yoyote juu ya pesa hizo.” Bi Rugut alisema Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Igonga ameamuru polisi wamrudishie Bw Muhinyuza kiasi hicho Dola 2.6 milioni. Bi Alego alisema serikali imeagiza pesa hizo zirudishwe kwa mwekezaji huyo aendelee na biashara na kubuni ajira kwa wakenya. Kabla ya polisi kuagizwa kurudisha pesa hizo Bw Koome alipinga ombi hilo akisema “apewe muda wa wiki mbili atafute wakili awasilishe ombi la kuzuia kutwaliwa kwa pesa hizo na Muhinyuza.” Bw Koome alisema : “nimewatimua kazini mawakili Cliff Ombeta, Jackson Omwanza na hivyo nahitaji muda wa kumtafuta wakili mwingine kwa vile sielewi ombi hili la DPP na madhara yake katika kesi hii inayonikabili.” Mahakama iliombwa na wakili Danstan Omari isitilie maanani ombi la Bw Koome kwa vile “pesa anazodai sio zake.” Bi Rugut alisema DPP hapingi pesa hizo zilizokuwa zimezuiliwa kama ushahidi katika kesi inayomkabili Bw Koome. Bi Rugut alisema Desemba 27, 2023, Bw Koome hajakata rufaa kupinga uamuzi wa kumng’oa katika kampuni ya SOL na agizo la kulipa fidia na kurudishia Muhinyuza Dola 100,000 alizomdanganya zilikuwa za kulipia kodi biashara ya SOL lakini “akazitia kibindoni.” Bi Alego alielezwa kesi inayomkabili Bw Koome ni kwamba alikula njama za kumlaghai Bw Muhinyuza kiasi Dola 2.6 milioni na wizi wa Dola 100,000. Mahakama ilikubalia ombi la DPP na kuagiza pesa hizo arudishiwe Muhinyuza. Sasa Bw Koome atapambana na hali yake na kesi ya ufisadi inayomkabili. Kesi inayomkabili Bw Koome itaanza kusikilizwa Februari 9, 2023. Alikana mashtaka manne ya ufisadi na wizi na yuko nje kwa dhamana ya pesa taslimu Sh500,000 You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na BENSON MATHEKA WALIOKUWA viongozi wakuu wa upinzani kabla ya handisheki wametajwa kama wasaliti wa mwananchi wa kawaida. Hii ni baada ya viongozi hao wakiongozwa na kinara wa ODM, Raila Odinga kumezwa na serikali ya Jubilee na hivyo sauti zao kuzimwa. Wanasiasa hao na wakuu wa mashirika ya umma sasa wanakula ronjoronjo huku maisha ya Wanjiku yakiendelea kuwa magumu kutokana gharama ya juu ya bidhaa, ukosefu wa ajira kwa vijana, ushuru wa juu, ufisadi, madeni, maafisa wa serikali kupuuza sheria miongoni mwa matatizo mengine. Hali ilibadilika tangu handisheki kwa kile Rais Uhuru Kenyatta na Bw Odinga walichotaja kuwa muafaka wa kuunganisha Wakenya. KUKOSA SAUTI Kulingana na wadadisi wa siasa, waliokuwa viongozi wa upinzani wakiongozwa na Bw Odinga wamekuwa wakitafuna minofu hivyo kukosa sauti ya kutetea Wanjiku. “Hakuna mtu anayepiga kelele au kuzungumza akitafuna kwa sababu ni tabia mbaya kufanya hivyo,” asema mdadisi wa masuala ya kisiasa Martin Andati. “Wamenufaika kwa kuacha kukosoa serikali. Kwa mfano, Bw Odinga ana wadhifa katika AU huku aliyekuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka akiwa balozi wa amani Sudan Kusini. Nyadhifa hizi zina marupurupu,” aeleza mdadisi wa masuala ya kisiasa Tom Maosa. “Kimya chao sio cha kushangaza. Hawakuwa katika upinzani kwa kupenda au kwa sababu ya imani na misimamo yao. Ni nafasi walikuwa wamekosa ya kufaidika kiuchumi,” asema Bw Maosa. Anatoa mfano wa Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ambaye alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali ya Jubilee kutoka Pwani, na majuzi ilifichuliwa kuwa anafaidika kibiashara kupitia kampuni zinazohusishwa na familia yake. Kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula pia amenyamaza. Aliyekuwa seneta wa Machakos Johnstone Muthama, ambaye ni mwandani wa karibu wa Bw Musyoka pia ameacha kukosoa serikali na amekuwa akiwahimiza viongozi kumuunga mkono Rais Kenyatta. Kimya cha upinzani kilipenya hadi bunge ambapo waliokuwa wakipaza sauti kukosoa serikali sasa ndio wapigaji debe wakuu wa Jubilee. Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Taifa, John Mbadi amekuwa akisikika tu anapoimba wimbo wa kiongozi wa wengi Aden Duale, tofauti na awali ambapo alikuwa akimkosoa vikali. Hali ni sawa katika Seneti ambapo James Orengo amekuwa mtetezi mkuu wa serikali ya Jubilee. Bw Orengo alipata kiti cha Kiongozi wa Wachache katika Seneti baada ya handisheki kufuatia kubanduliwa kwa Bw Wetangula. Wabunge wengine ambao wamezima sauti ni Millie Odhiambo (Mbita), Peter Kaluma (Homa Bay Mjini ), Otiende Amollo (Rarienda), Opiyo Wandayi (Ugunja), Gladys Wanga (Mwakilishi wa Wanawake Homa Bay) na T.J. Kajwang (Ruaraka). Wadadisi wanasema japo wamekuwa wakidai kwamba waliamua kuunga mkono handisheki ili kutuliza joto la kisiasa, ukweli ni kuwa wanafaidika binafsi ndiposa wakanyamaza. MANUFAA Anasema walichofanya wanasiasa wa upinzani ni kujiunga na Bw Odinga ili wapate kunufaika hata kama hawakubaliani na maoni yake. Sauti za viongozi wa mashirika ya kijamii ambao walikuwa wakikosoa serikali pia zilididimia baada ya muafaka. Bw Andati anasema wanaharakati wengi walivutwa upande wa serikali na wachache waliobaki wakaingizwa baridi. Kulingana na ripoti ya Uwazi Consortium iliyotolewa Mei mwaka huu, handisheki ndiyo iliyozima mashirika hayo. Wanaharakati waliokuwa wakilaumu serikali kama vile Gladwel Otieno wa shirika la AfriCog, George Kegoro na Profesa Makau Mutua wa Kenya Human Rights Commission na Maina Kiai wa InformAction wamekuwa kimya. Dkt Kennedy Orengo wa Uwazi Consortium alisema japo handisheki ilituliza joto la kisiasa, kwa upande mwingine imelemaza kustawi kwa demokrasia kwani ulimaliza upinzani. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

It looks like nothing was found at this location. Maybe try one of the links below or a search? Try looking in the monthly archives. 🙂 © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA BRIAN OKINDA [email protected] KAMPUNI ya Sportpesa imejiunga na baadhi ya kampuni zingine za kamari nchini zilizoruhusiwa kurejelea kutekeleza shughuli zao za bahati nasibu baada ya kuzuiliwa kufanya hivyo kwa muda. Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini, KRA Jumanne iliidhinisha kurudishwa kwa leseni ya kampuni hiyo baada ya kuzimwa kwa muda wa miezi miwili. Katika ujumbe uliotumwa kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo ilisema kuwa imekuwa ikijadiliana na washikadau, na pia wadhibiti wa ushuru kutoka kwa serikali kuhusu leseni yake, majadiliano ambayo yalinuia kueleza vyema madhumuni na sheria ambazo zinahitajiwa kufuatwa, ikiwemo ile ya kulipa ushuru. “Tumekuwa na majadiliano ambayo yamenawiri na tuna furaha kuwa shirika la kutoza ushuru nchini limekubali kutupea upya leseni yetu. Tuna imani kuwa majadiliano haya yote yatakamilika hivi karibuni ili tuweze kuendelea na shughli zetu za awali,” ujumbe wa Sportpesa ulisema. Taarifa hiyo ilizidi kueleza kuwa kampuni hiyo inawashukuru wafanyikazi na mashabiki wake wote, na hivi karibuni, itatoa ujumbe kueleza itakapokua ikirejelea shughli zake. “Sportpesa inaahidi kujitolea kwake kusaidia jitihada za serikali kutekeleza maendeleo nchini, kwa kuendeleza shugli zake ikizingatia sheria za serikali ikiwemo ile ya kutoa ushuru,” taarifa hiyo ilisema. Kampuni hiyo ya kamari ilikua miongoni mwa zingine zikiwemo Betin, Betway, Betpawa, Premierbet, Lucky 2U, 1XBet, Mozzartbet, Dafabet, World Sport Bet, Atari Gaming, Palmsbet, Bet Boss, Betyetu, Elitebet, Bungabet, Cysabet, Nestbet, Easybet, Kick Off, Millionaire Sports Bet, Kenya Sports Bet na Eastleighbet, ambazo leseni zao zilifutiliwa mbali na serikali mwezi Julai, kwa shutuma za kutolipa ushuru. Serikali ilidai kuwa kampuni hizi zilikuwa zinapata faida ya kiasi cha Sh200 bilioni kila mwaka ila yalitoa ushuru wa shilingi Sh4 bilioni tu, mwaka uliopita. Mkurugenzi mkuu wa Sportpesa, Ronald Karauri, hata hivo alikana madai haya, hasa ile inayohusu kiwango cha ushuru. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na JEREMIAH KIPLANG’AT NAIBU Rais William Ruto ameonekana kukumbatia mtandao wa Twitter katika siku za hivi karibuni kila anapotaka kukanusha taarifa zozote zinazoonekana kumharibia jina, hasa kutoka kwa vyombo vya habari. Mkakati wake umefasiriwa kuiga ule wa Rais Donald Trump wa Amerika, ambaye amekuwa akitumia mtandao huo kuwakabili watu anaowachukulia kuwa mahasimu wake kisiasa ama vyombo vya habari vinavyoandika taarifa zinazomkasirisha. Mnamo Jumapili mwendo wa saa tano usiku, Dkt Ruto alitumia akaunti yake ya Twitter kukanusha habari zilizoangaziwa na gazeti moja nchini kumhusu. Kwenye ujumbe alioandika, Dkt Ruto aliweka picha yenye kichwa cha habari kuu za gazeti hilo, zilizohusu madai kwamba Rais Uhuru Kenyatta alimkwepa katika Uwanja wa Kitaifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) aliporejea nchini kutoka Japan mnamo Alhamisi iliyopita. “Chama cha Jubilee kimejengwa kwa msingi thabiti hivi kwamba, hakuna njama zozote ama propaganda zitakazokisambaratisha,” ukaeleza ujumbe huo. Ilikuwa ni mara ya pili chini ya wiki moja kwa Dkt Ruto kutumia mtandao huo kupuuzilia habari zilizochapishwa na vyombo vya habari kumhusu. Ana ufuasi wa watu 2.3 milioni kwenye mtandao huo. Mwezi uliopita, alipuuzilia mbali habari kuu za gazeti lingine kuwa washirika wake wa kisiasa walikuwa wakipanga kupinga kura ya maoni kuhusu mageuzi ya kikatiba inayotarajiwa kupendekezwa na Jopo la Maridhiano (BBI) lililobuniwa na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga. Kabla ya kuanza kutumia mitandao ya kijamii, Dkt Ruto alikuwa akipuuzilia mbali baadhi ya habari zinazomhusu, ambapo mara nyingi aliwategemea washirika wake kuzikanusha. Katika nyakati zingine, alikuwa akikanusha habari hizo kwenye mikutano ya umma. Kwa sasa, mtandao huo unaonekana kuwa jukwaa lake analopendelea zaidi. Jana, Msimamizi Mkuu wa Mawasiliano katika afisi ya Naibu Rais, Bw David Mugonyi alisema Dkt Ruto anaamini katika uhuru wa vyombo vya habari, ambapo ndipo ameamua kuvituamia ili kujielezea. “Naibu Rais anaamini katika uwepo wa vyombo vya habari. Hilo linajumuisha haki ya kufanya makosa, lakini si kubuni habari za uongo kwa malengo ya kisiasa. Hiyo ndiyo sababu kuu ambapo bado hajavishtaki vyombo hivyo, licha ya kuwa na haki ya kisheria kufanya hivyo. Badala yake, amechagua njia ya kueleza ukweli kupitia mitandao ya kijamii,” akasema Bw Mugonyi. Hata hivyo, Naibu Afisa Mkuu Mtendaji wa Bazara la Vyombo vya Habari Kenya (MCK) Bw Victor Bwire alisema kuwa Dkt Ruto anapaswa kutumia mkondo wa kisheria kueleza matatizo yoyote dhidi ya vyombo vya habari. “Naibu Rais ana haki ya kueleza tatizo lolote alilo nalo dhidi ya vyombo vya habari. Ni haki yake kufanya hivyo. Tungependa kumshauri atumie taratibu za kisheria. Tuko tayari kutathmini uhalali wa malalamishi yake,” akasema Bw Bwire, kwenye mahojiano na ‘Taifa Leo.’ Mnamo Jumatatu, Bw Trump alivikashifu vikali vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiandika taarifa za kumharibia jina. Rais huyo ametoa matamshi ya kudhalilisha waandishi hasa katika kipindi hiki nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na WANDERI KAMAU CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu Kenya (KUSU) kinamtaka Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara Prof Mary Walingo kujiuzulu kutokana na madai ya ufujaji wa mamilioni ya pesa. Madai hayo yalifichuliwa na taarifa ya kipekuzi iliyopeperushwa na runinga ya Citizen mnamo Jumapili, ambapo inadaiwa kuwa zaidi ya Sh190 milioni zilifujwa kwa maagizo ya msimamizi huyo tangu mwaka 2016. Kwenye kikao na wanahabari jijini Nairobi jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Charles Mukwaya alisema kuwa mkuu huyo anapaswa kujiondoa ili kuruhusu uchunguzi kuendelea au ashurutishwe kujiondoa na asasi za serikali. “Tunamtaka Prof Walingo kujiuzulu ili kutoa nafasi ya uchunguzi kamili kuhusu madai hayo. Lazima ajiondoe ili kuwapa nafasi asasi husika nafasi ya kuendesha uchunguzi wao bila vikwazo vyovyote,” akasema Dkt Mukwaya. Mnamo Jumatatu, maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) walifika katika chuo tayari kuanza uchunguzi wao. Kulingana na DCI, baadhi ya wafanyakazi tayari wameandikisha taarifa kuhusiana na sakata hiyo. Chama pia kiliziomba idara za usalama kuimarisha ulinzi wa wafanyakazi waliofichua kashfa hiyo, wakisema kuwa huenda wakaanza kupokea vitisho. “Ufichuzi huo umefanywa na wafanyakazi wa ngazi za chini chuoni, hivyo lazima serikali iwahakikishie usalama wao kwani kuna uwezekano kuwa watatishiwa na watu wanaodaiwa kuhusika katika sakata hiyo,” akasema. Chama hicho vilevile kiliiomba serikali kutoangazia chuo hicho pekee, bali vyuo vyote vya umma nchini, ili kurejesha hali ya uwajibikaji, hasa usimamizi na matumizi ya fedha zinazotengewa. Kilidai kuwa kimelalamikia usimamizi na matumizi ya pesa katika vyuo vikuu vya Masinde Muliro, Embu kati ya vingine. Kulingana na ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, chuo hicho hakikueleza vile kilitumia Sh16.8 milioni za wanafunzi 494 licha ya kutowajumuisha kwenye sajili rasmi ya wanafunzi wake katika mwaka wa matumizi ya fedha za serikali wa 2015/206. Chuo vile vile kilikosa kueleza kilivyotumia Sh12 milioni za mikopo ya wanafunzi, kwani kilipokea Sh72 milioni kutoka kwa Bodi ya Elimu ya Juu (HELB) licha ya kuomba Sh60 milioni. Kwenye mojawapo ya video zilizorekodiwa kisiri, mkuu huyo anasikika akiwatishia wafanyakazi wake kwamba “watazama naye ikiwa ataenda gerezani.” You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na AFP na MARY WANGARI JOHANNESBURG, Afrika Kusini WAZIRI Mkuu David Makhura amesema mashambulizi ya ubaguzi wa rangi hayataruhusiwa Gauteng, Afrika Kusini na kuitisha utulivu katika maeneo yaliyoathiriwa huku polisi wakiimarisha doria kufuatia visa vya ghasia na uporaji. Matamshi yake yalijiri huku Serikali ya Nigeria ikitaja mashambulizi hayo kama yasiyofaa ambapo Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amepanga kukutana na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa mnamo Oktoba kuhusiana na kuongezeka kwa mashambulizi hayo. Hata hivyo, Makhura alisema hataomba msamaha kwa raia wa kigeni wanaoshiriki uhalifu, akidokeza kwamba kufikia sasa, polisi wanaendelea kupambana visa vya uporaji na uhalifu mkoani humo na kwamba hali ilikuwa shwari. “Hatuwezi kuwachukulia raia wote wa kigeni kama wahalifu na wale wanaohusika katika uhalifu ni sharti wakabiliwe. Kila mtu ni sharti atii sheria awe raia wa taifa hili au wa raia wa kigeni, “alisema Makhura. Alisema vitendo vya uporaji haviwezi kutetewa kwa ukosefu wa ajira na visa vya uhalifu akisema hatafidia wamiliki wote wa duka ambao wamepoteza mali yao. Kulingana na Makhura, Afrika Kusini inakabiliana na raia wa kigeni haramu ambao hawajasajiliwa huku akiahidi kuimarishwa kwa usalama mipakani kuhakikisha eneo hilo lina utulivu. Kiongozi wa Economic Freedom Fighters (EFF) Julius Malema, alitoa hakikisho kwamba Afrika Kusini ni ya watu wote huku akilaani kuzuka kwa mashambulizi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa kigeni nchini humo. Rais wa Muungano wa Nigeria Afrika Kusini (NUSA), Adetola Olubajo aliyethibitisha maendeleo hayo kwa vyombo vya habari alisema mashambulizi hayo yalianza mnamo Jumapili asubuhi eneo la Jeppestown mjini Johannesburg wakati jumba liliteketezwa na umati uliojawa na ghadhabu. Malema alitoa wito wa kukomesha mashambulizi hayo dhidi ya raia wa kigeni akisema Afrika Kusini ni ya watu wote. Katika taarifa aliyotia sahihi, Malema pia alipuuzilia mbali madai kwamba raia wa kigeni walikuwa wakichukua kazi zinazostahili kupatiwa wananchi wa Afrika Kusini. “Uwe umetoka Afrika Kusini, au umetoka Zimbabwe, ama umetoka Nigeria, hapa ni nyumbani kwako. “Hakuna ajira katika taifa la Afrika Kusini kwa sababu Wamagharibi wanakataa kuwekeza fedha Afrika Kusini, wana akiba nyingi mno kwenye benki. “Wakati ni mzungu nchini Afrika Kusini ambaye hajasajilishwa anaitwa mwekezaji, ikiwemo raia wa India na Uchina. Lazima kujichukia sisi wenyewe kukome!” “Afrika sisi ni wamoja. Raia wa Nigeria ni kaka zetu. Acha tuvumiliane.” You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA ERICK MATARA MJADALA kuhusu mpango wa serikali wa kuwafurushwa watu kwenye msitu wa Maasai Mau Jumatatu uliendelea kuchacha, viongozi na wazee kutoka Bonde la Ufa sasa wakiomba kuandaa mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kuhusu operesheni inayonukia baada ya makataa ya Oktoba 31. Mbunge wa Kuresoi Joseph Tonui, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee kutoka Bonde la Ufa Gilbert Kabage na Kinara wa wazee wa Ogiek Joseph Towett walisema ni Rais Kenyatta pekee ambaye anaweza kuyaokoa maisha ya maelfu ya raia ambao wanakodolewa macho na mahangaiko makubwa serikali ikiwaondoa msituni humo. “Tutafanya kila tuwezalo kukutana na Rais Uhuru Kenyatta na kusuluhisha utata huu ambao umeibua taharuki kati ya jamii mbalimbali. Iwapo suala hili halitatuliwa basi kutatokea janga kubwa la kibinadamu litakalowaathiri watahiniwa wa mitihani ya kitaifa mwaka huu,” akasema Bw Tonui. Mbunge huyo wa chama cha Jubilee aliongeza kuwa hatima ya wanafunzi 8,000 na watahiniwa 1,000 sasa ipo mikononi mwa Rais na kumwomba aunde jopo la wataalamu ili kupendekeza suluhu kwa masuala tata yanayozingira msitu huo kila mara. Kwa upande wake, Mzee Towett alisema wanaunga kikamilifu juhudi za kuhifadhi msitu huo unaotegemewa na mamilioni ya watu ila akaomba serikali kushughulikia suala hilo kwa makini bila kudhuru raia. “Ili kuzima taharuki ya kijamii inayoendelea kupanda kati ya jamii zinazoishi kwenye msitu, serikali lazima iunde jopo la wataalamu kusuluhisha utata wa ardhina dhuluma za kihistoria ndani ya Mau,” akasema Mzee Towett. Wito wa kumtaka Rais Kenyatta kuingilia suala hilo linajiri baada ya viongozi wa jamii ya Kalenjin wiki jana kumwomba Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko kuwa na kikao nao huku serikali ikiwapa zaidi ya familia 60,000 muda wa siku 60 kuondoka msituni au zifurushwe kwa nguvu. Bw Kabage naye alilaumu utawala wa Rais Mstaafu Daniel Moi kwa hali ya sasa akisema kuruhusiwa kwa jamii moja kujitwalia vipande vikubwa vya ardhi ndiyo kiini cha uhasama wa kikabila msituni humo. “Umefika wakati ambao suala hili la Mau linafaa kutatuliwa mara moja badala ya kuwaacha wanasiasa kulitumia kila mwaka wa uchaguzi kutafuta kura,” akasema Bw Kabage. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA AFP VIONGOZI wa Baraza jumuishi la uongozi nchini Sudan, jana walimtembelea aliyekuwa Rais Omar al-Bashir katika gereza maarufu la Kobar, Kaskazini mwa Khartoum anakoendelea kuzuiliwa baada ya kuondolewa mamlakani mwezi Aprili mwaka huu. Kiongozi wa baraza hilo Aisha Mousa na ujumbe wake walimtembelea Bashir pamoja na wafungwa wengine wa kisiasa kama njia ya kuthibitishia raia wa Sudan kwamba viongozi hao wa utawala uliopita bado wapo kizuizini. Kulingana na taarifa rasmi kutoka kwa Mousa, viongozi 23 ambao walikuwa kwenye serikali ya Bashir wanaendelea kuzuiliwa wakingoja kuhukumiwa kwa makosa mbalimbali. Mousa pia alifichua kwamba ujumbe huo uliandaa mazungumzo ya kina na Bashir na kumhakikishia kwamba mchakato wa kupata haki hautaingiliwa kivyovyote kisiasa. Wakati uo huo, mawaziri wa kuhudumu kwenye baraza hilo wanatarajiwa kutajwa wiki hii. Duru ndani ya baraza hilo zilieleza kwamba mashauriano kuhusu viongozi wa kuteuliwa kuhudumu kwenye serikali yamekamilika na kilichosalia ni kutangazwa pekee. Habari hizo zilifafanua kwamba orodha ya majina ya mawaziri iliyowasilishwwa na Chama cha Upinzani (FCA) kwa Baraza la Mpito la Jeshi(TMC) iliidhinishwa na hakuna jina lolote lililokataliwa. Vilevile mkutano kati ya maafisa wa FCA pamoja na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok jana ulifanyika lengo kuu ikiwa kuorodhesha wasifu wa mawaziri wapya kabla ya kuyatangaza majina yao rasmi. Serikali itakayoongozwa na Hamdok itawajumuisha mawaziri 19 na wanachama watano wa mabaraza makuu. Baraza jipya la mawaziri lilitarajiwa lizinduliwe Jumamosi na kuapishwa Jumapili lakini kukaibuka tofauti chache ambazo zilichangia tangazo hilo kutotolewa kabla ya makataa ya Agosti 31. Ziara ya Mousa na kundi lake lilijiri siku moja tu baada ya Bashir kushtakiwa kwa kutumia na kupata fedha za kigeni kwa njia ya haramu, makosa ambayo huenda yakamvutia kifungo cha miaka 10. Akiwa mbele ya mahakama kwa kikao cha tatu cha kusikiza kesi yake, Jaji Al-Sadiq Abdelrahman aliorodhesha mashtaka matatu yanayomkabili Bashir. “Maafisa wa usalama wa serikali walipata Sh2.5 bilioni nyumbani kwako ambazo ulipokea na kutumia kwa njia zisizofaa,” akasema Jaji Abdelrahman. Hata hivyo, Bashir alijitetea na kueleza korti kwamba alipokea pesa hizo kutoka Mwanamfalme wa Saudia Mohamed bin Salman huku wafuasi wake na jamaa zake wakiimba ‘Allahu Akbar’ kama njia ya kumtia moyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na PIUS MAUNDU GAVANA wa Makueni, Prof Kivutha Kibwana amepuuzilia mbali madai ya baadhi ya wandani wa kinara wa chama cha, Bw Wiper Kalonzo Musyoka kuwa amejiunga na mrengo wa TangaTanga unaompigia debe Naibu Rais, Dkt Rais William Ruto. Prof Kibwana ambaye amejiunga na orodha ya wanaowania Urais mwaka wa 2022, amesema madai kwamba amejiunga na kambi ya Dkt Ruto yanaenezwa na watu wanaohofia umaarufu wake eneo la Ukambani. Madai hayo yalienea majuma mawili yaliyopita baada ya Prof Kibwana kuandamana na Naibu Rais kwenye ziara ya kiserikali katika kaunti ya Turkana. Prof Kibwana ambaye anahudumu kipindi chake cha pili, aliwaacha viongozi wengine vinywa wazi, aliposema uwaniaji wa Dkt Ruto haufai kupuuzwa na pia kumrai kumaliza uhasama kati yake na Kiongozi wa ODM Raila Odinga. Ni kutokana na matamshi hayo ambapo wandani wa Bw Musyoka, walimchemkia gavana huyo huku kinara wao pia akikabiliwa na ushindani kutoka kwa Gavana wa Machakos Dkt Alfred Mutua ambaye pia ametangaza kuwa atakuwa debeni 2022. Mbunge wa Makueni Daniel Maanzo, Jumamosi aliambia mkutano wa kisiasa katika Shule ya Upili ya Mathemba kwenye eneobunge lake kwamba Prof Kibwana ni ajenti wa Dkt Ruto eneo la Ukambani. “Gavana amejiunga na mrengo wa Tangatanga akiwa na nia ya kumdunisha Bw Musyoka. Hatutamruhusu mtu yeyote hapa Ukambani kuwania Urais dhidi ya Bw Musyoka,” akasema, akiunga kauli ya aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama na Seneta wa Kitui Enock Wambua. Viongozi hao wanaamini kwamba Bw Mutua na Prof Kibwana watagawanya kura chache za jamii ya Wakamba na kuhatarisha azma ya Bw Musyoka ya kuingia ikulu 2022. Hata hivyo, Prof Kibwana amekanusha kwamba yupo Tangatanga, akisema havumishi uwaniaji wa Dkt Ruto. “Chama cha Wiper hakitakuwa maarufu kwa kueneza propaganda,” akaeleza Taifa Leo jana. Gavana huyo ambaye amejizolea sifa kwa kuendeleza ugatuzi kwa njia ya kustaajabisha eneo la Makueni, alivuliwa uenyekiti wa chama cha Wiper kutokana na msimamo wake. Baraza Kuu la chama hicho majuzi liliidhinisha aliyekuwa mbunge wa Matuga, Chirau Ali Mwakwere awe mwenyekiti wake mpya. Matamshi hayo makali ya kisiasa yanajiri baada ya Prof Kibwana kukutana na Kinara wa ANC Musalia Mudavadi, akimwomba amlinde dhidi ya shutuma kali ya wandani wa Bw Musyoka. “Unafaa kutufundisha mtindo wa kisiasa ambao unaendelezwa Magharibi mwa Kenya ili mimi, Bw Musyoka na Dkt Mutua wakieleza nia ya kuingia ikulu, basi hakuna atakayeonekana kuwa msaliti mwenye nia ya kumharibia mwenzake,” akasema Prof Kivutha. Kwa upande wake, Bw Mudavadi aliwaomba wandani wa Bw Musyoka kuruhusu demokrasia itambe ukambani na kukoma kuwadunisha wanaopinga azma ya makamu huyo wa zamani wa Rais. Bw Mudavadi ambaye pia ametangaza azma ya kuwania Urais 2022, alisema kwamba hakuna tatizo lolote iwapo magavana hao wawili wangependa kutoa upinzani kwa Bw Musyoka. “Hakufai kuwe na uhasama wowote iwapo wanasiasa kutoka eneo moja wangependa kuwania Urais 2022,” akasema Bw Mudavadi mjini Wote baada ya kuandaa mazungumzo ya kina na Prof Kibwana katika afisi za kaunti. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MHARIRI |
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI |
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI |
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI |
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI |
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI |
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI |
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI |
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI |
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI |
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini. |
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI |
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI |
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na BENSON MATHEKA |
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU |
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA |
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA |
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA |
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU |
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA |
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO |
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI |
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA |
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON |
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA |
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na MASHIRIKA |
LONDON, Uingereza |
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB |
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA |
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO |
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU |
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO |
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI |
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde |